Watu Aina Saba Watakaokuwa Katika Kivuli Cha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Siku Ya Qiyaamah
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna watu saba (7) ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atawafunika katika kivuli chake katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)”:
1. Kiongozi Muadilifu;
2. Kijana aliyekulia katika kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa);
3. Muislamu ambaye moyo wake umesehelea katika msikiti;
4. Watu wawili wapendanao kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), Kukutana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kuachana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa);
5. Mwanaume aliyeitwa na mwanamke mrembo kwa kutaka kufanya matendo ya haramu na akasema, “La hakika mimi namuogopa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa)”.
6. Mtu anayetoa sadaka kwa mkono wa kulia na wa kushoto usijue kitu kilichotendeka (atoae sadaka kwa siri bila ya wengine kujua kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na
7. Mtu anayemkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa faragha na huku macho yake yakatokwa na machozi.”
[Al-Bukhaariy na Muslim]
No comments:
Post a Comment