Karibu katika blog hii kwa kupata nasheed , qur an na vinginevyo vinavyohusu dini ya uislamu unaweza kupata video zetu kupitia channel yetu ya youtube ambayo ni Maulid Bin Swaleh pia usisahau kusubscribe yetu(Welcome in this blog to get qaswida , nasheed , qur an ,and others inside the islamic)
Kufunga siku ya tisa (9) na kumi (10) ni bora zaidi kuliko kufunga siku ya kumi (10) na ya kumi na moja (11)
صيام التاسع مع العاشر أفضل من صيام الحادي عشر مع العاشر.
*KUFUNGA (SIKU) YA TISA (9) NA KUMI (10) NI BORA ZAIDI KULIKO KUFUNGA SIKU YA KUMI (10) NA YA KUMI NA MOJA (11).*
للعلامة الإمام عبد العزيز بن عبد الله بن باز- رحمه الله-
*(Fatwa) ya Mwanachuoni Mkubwa 'Abdul-'Aziiz bin 'Abdullah bin Baaz-Allah amrahamu-*
السؤال:
*Suali: 🎤*
ما حكم صيام يوم عاشوراء، وهل الأفضل صيام اليوم الذي قبله أم اليوم الذي بعده أم يصومها جميعا أم يصوم يوم عاشوراء فقط ؟ نرجو توضيح ذلك جزاكم الله خيرا.
*Ni ipi hukumu ya kufunga 'Aashuraa, na je ni bora zaidi kufunga siku ambayo inayofuata au siku (moja) kabla yake au afunge (siku) zote au afunge 'Aashuraa peke yake?*
نرجو توضيح ذلك جزاكم الله خيرا.
*Tunataraji ufafanuzi wa hilo Allah awalipe kheri.*
الجواب:
*Jawabu: 📚*
صيام بوم عاشوراء سنة؛
*Kufunga siku ya kumi ya mwezi wa Muharram (mfungo nne) ni sunnah,*
لما ثبت في الأحاديث الصحيحة عن رسول الله- صلى الله عليه وسلم من الدلالة علــے ذلك،
*Kwa sababu ya hadithi sahihi sa mtume- swala na salamu zimfikie-zinazojulisha hilo,*
وأنه كان يوما تصومه اليهود،
*Na hakika hiyo (siku) ni siku (ambayo) Mayahudi walikuwa wakiifunga,*
لأن الله نجى فيه موسى وقومه وأهلك فرعون وقومه،
*Kwa sababu Allah alimuokoa (ndani ya siku hiyo) Musa na watu wake na alimwangamiza Firauni na watu wake,*
فصامه نبينا محمد - صلــے الله عليه وسلم شكرا لله، وأمر بصيامه،
*Basi akafunga nabii wetu Muhammad kwa kumshukuru Allah, na akaamrisha ifungwe,*
وشرع لنا أن نصوم يوما قبله أو يوما بعده،
*Na akatuwekea (kuwa) ni sunnah tufunge siku (moja) kabla yake au siku (moja) baada yake,*
وصوم التاسع مع مع العاشر أفضل،
*Na kufunga (siku) ya tisa na ya kumi ni bora zaidi,*
وإن صام العاشر مع الحادي عشر كفــے ذلك، لمخالفة اليهود،
*Na kama (mtu) akifunga siku ya kumi na ya kumi na moja hilo linatosha kwa ajili ya kwenda kinyume na Mayahudi,*
وإن صامهما جميعا مع العاشر فلا بأس؛
*Na kama atazifunga (siku) mbili zote (9+11) pamoja na siku ya kumi basi (hilo) halina ubaya,*
لما جاء في بعض الروايات:
*Kwa sababu ya (maneno) yaliyokuja katika baadhi ya riwaya (ambayo) ni:*
”صوموا يوما قبله ويوما بعده“
*“Fungeni siku (moja) kabla yake na siku (moja) baada yake”*
أما صومه وحده فيكره والله ولي التوفبق.
*Ama kuifunga ('Aashuraa) peke yake inachukiza, na Allah ndiye msimamizi wa taufiq.*
📚 المصدر: مجموع فتاوى ابن باز (404/15)
*[ Chanzo: Maj'mu'u fataawa ibn Baaz (15/404) ]*
*Mfasiri: Abuu Thurayyaa Ismail seiph Mbonde - Allah amuhifadhi*
Dar es salaam, Tanzania 🇹🇿
Watu wa aina saba watakaokuwa katika kivuli cha ALLAH
Watu Aina Saba Watakaokuwa Katika Kivuli Cha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Siku Ya Qiyaamah
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kuna watu saba (7) ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atawafunika katika kivuli chake katika siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)”:
1. Kiongozi Muadilifu;
2. Kijana aliyekulia katika kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa);
3. Muislamu ambaye moyo wake umesehelea katika msikiti;
4. Watu wawili wapendanao kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), Kukutana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kuachana kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa);
5. Mwanaume aliyeitwa na mwanamke mrembo kwa kutaka kufanya matendo ya haramu na akasema, “La hakika mimi namuogopa Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa)”.
6. Mtu anayetoa sadaka kwa mkono wa kulia na wa kushoto usijue kitu kilichotendeka (atoae sadaka kwa siri bila ya wengine kujua kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na
7. Mtu anayemkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa faragha na huku macho yake yakatokwa na machozi.”
[Al-Bukhaariy na Muslim]
Shariy’ah Ya Dini ImekamilikaImaam Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah)
Shariy’ah Ya Dini Imekamilika
Imaam Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:
Shariy’ah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni shariy’ah iliyokamilika kabisa, haikuacha jambo lolote jema lililojulikana na werevu isipokuwa ameliamrisha. Na hakuacha jambo lolote lillilokua ovu na ambalo limejulikana na werevu isipokua amelikataza. Hakuamrisha jambo na watu wakasema "Laiti kama asingeliamrisha". Na Hakukataza jambo wata wakasema "Laiti kama asingelikataza"
[Al-Bidaayah Wan-Nihaayah (6/79)]
Kuigawa dini katika misingi na matawi.
Kuigawa Dini Katika Misingi Na Matawi
Shaykh ‘Abdullaah Al-Ghunaymaan
Kuigawanya Dini kwenye misingi mikuu (uswuul) na matawi (furuu).
Misingi mikuu ya Dini (uswuul) sio ya kidhanifu au kinadharia pekee, wala hakuna utenganifu baina ya iymaan na vitendo ndani ya Uislaam.
Hakuna chochote ndani ya Qur-aan au Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayopendekeza kwamba misingi mikuu ni ya iymaan tu pekee na kwamba misingi midogo ni ya vitendo pekee.
Asili ya utenganifu huu umetokana na Mu’tazilah (na wafuasi wao), ambao ndio waliotenganisha namna hii: misingi mikuu na matawi.
[Shaykh ‘Abdullaah al-Ghunaymaan]
Aina nne za jihad.
Aina Nne Za Jihaad
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
Jihaad ni aina nne:
Jihaad ya (kukabiliana na) nafsi, jihaad ya (kupambana na) shaytwaan, jihaad ya (kupambana na) makafiri, jihaad ya (kukabiliana na) wanafiki.
[Zaad Al-Ma’aad (3/9)]
Haki za mume na mme.
Imekusanywa na: Ummu Iyyaad
Haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللّهُ عَزِيزٌ حَكُيمٌ
Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah). Na kwa wanaume juu ya hao wanawake wana daraja. (Al-Baqara 2: 228)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema katika Hijjah ya kuaga aliposimama kuwahutubia Maswahaaba:
((يآ أيُّهَا النَّاسُ إِنَّ لِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقاً وَلَكُمْ عَلَيْهِنَّ حَقّ)) أبو داود
((Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu)) Abu Daawuud
Zifuatazo ni haki zinazowahusu wote wawili; mke na mume katika kuamiliana:
1-Ukweli
Mke na mume wawe ni wakweli baina yao kwa kauli na vitendo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ
Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. (At-Tawbah: 11)
2-Mapenzi, huruma na utulivu.
Kila mmoja amdhihirishie mwenziwe mapenzi, na wawe na huruma baina yao katika shida na matatizo mpaka iwe kila mmoja awe ni kutulizo cha mwenziwe wakati wa dhiki. Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) Anasema:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَة ًإِنَّ فِي ذَلِكَ لَآ يَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
“Na katika Aayaat Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaotafakari.”(Ar-Ruwm 30: 21)
3-Amana, Uaminifu na kutumiza ahadi:
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amewasifu na kuwaahidi Jannah wanaotimiza amana na ahadi zao:
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ
|
Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (wanazitimiza). [Al-Muuminuwn 8] (Al-Ma’aarij: 32)
|
Kuweko uaminifu kutazuia dhana mbaya au kutiliana shaka:
فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ
Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah Mola wake (Al-Baqarah: 283)
4-Tabia njema
Wawe na tabia njema katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao:
وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
Na kaeni nao kwa wema ((An-Nisaa 4: 19))
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akausia:
((Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake)) Al-Bukhaariy na Muslim
5-Kuhifadhiana siri
Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao nje:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwenda kwa mume wake kisha (mmojawao) akapita kutoa siri yake)) Muslim
Haki hizo zitakapotimizwa kwa mume na mke, itakuwa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
وَلاَ تَنسَوُاْ الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). (Al-Baqarah 2: 237)
Haki za mke kutoka kwa mume:
1-Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe kumvisha na kumtimizia mahitaji yake.
2-Mume ana haki kumfunza adabu mke anapohisi mke anamuasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا
Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa). (An-Nisaa 4: 34)
Aayah hiyo inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo kuhusu: ((wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni)).
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) na wengineo wamesema: “Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali” (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al-Baswriy kasema: “Ina maana mpigo usio wa nguvu”.
Wanavyuoni wamefafanua kuhusu kauli hiyo ifautavyo:
i) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Mke atakapomtii mumewe, itosheleze kuwa matatizo yamekwisha.
ii) Atakapoendelea mke kutokumtii mume wake, basi mume ajitenge naye kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya na atambue kuwa mumewe amamekasirikia. Pindi mke akikubali makosa yake, yaishe matatizo na warudiane katika hali yao ya kawaida.
iii) Ikiwa bado mke hana utiifu, hapo mume anaweza kufuata amri hiyo ya kipigo. Lakini sio kumpiga kwa nguvu bali kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:
عن جابر (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم: أنه قال في حجة الوداع: ((واتَّقُوا اللهَ في النِّساءِ، فإنهن عندكم عَوَانٌ، ولكم عليهن ألا يُوطِئْنَ فُرُشكم أحدا تكرهونه، فإن فَعَلْن فاضربوهن ضَرْبا غير مُبَرِّح، ولهن رزْقُهنَّ وكِسْوتهن بالمعروف))
Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: ((Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha)) Muslim
3-Ni wajib wa mume kumpatia mafunzo ya Dini mke wake ikiwa mke hakujaaliwa kupata elimu ya Dini yake. Mume amfundishe mwenyewe, na pindi asipoweza, amruhusu mke kuhudhuria darasa kwa sababu ni muhimu kwake apate kujifunza yanayopasa kama ‘Aqiydah na Tawhiyd na ajiepushe na shirki. Pia ajifunze Fiqhi na yote yanayohusiana na Dini yake, aweze kutekeleza ibaada zake sawasawa na pia apate kuitakasa nafsi yake na aweze kujiepusha na maasi na aweze kulea watoto wake. Kwa ujumla aihami familia yake na Moto wa Jahannam. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaamrisha hivyo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾
Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto (ambao) mafuta (kuni) yake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa. (At Tahriym 66: 6)
4-Ni wajibu wa mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata Shariy’ah za Dini; mfano mke asipotimiza hijaab. Vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa ambao kaharimishwa nao kuolewa.
5-Ni wajibu wa mume kumhifadhi mke kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi na msimamizi wa mambo yake na ndiye mwenye majukumu ya kumhudumia:
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ
Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao. (An-Nisaa 4: 34)
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake)) Al-Bukhaariy na Muslim
6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anakataza kutokufanya uadillifu:
وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ
Na wala hamtaweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msielemee muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mke mwengine (msiyempenda) kama kining’inio (aliyetundikwa). (An-Nisaa 4: 129)
Na Anasema:
فَإِنْ خِف ْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ذَلِكَ أَدْنَى أَلاَّ تَعُولُواْ
Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki (masuriya). Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea (kudhulumu). (An-Nisaa 4: 3)
Juu ya hivyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameusia wanawake watendewe mema:
((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu)) At-Twabaraaniy
Haki za Mume kutoka kwa Mke:
1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:
((لَوْ كُنْتُ آمِراً أَحَداً أَنْ يَسْجُدَ لأِحَدٍ لأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقَّهِ عَلَيْهاَ))
((Ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake)) Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr
2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:
((إذا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلىَ فِرَاشِهِ فَأَبَتْ عَلَيْه لَعَنَتْهَا الْمَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ))
((Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi)) Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy
3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
((لاَ تُنْفِقُ الْمَرْأَةُ شَيْئًا مِنْ بَيْتِهَا إِلا بِإِذْنِ زَوْجِهَا)) قالوا: "يا رسول الله! وَلا الطَّعَامَ؟ قال: ((ذَاكَ أَفْضَلُ أَمْوَالِنَا)) صحيح ابن ماجه - حديث حسن الألباني
((Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe)). Wakasema: “Hata chakula ee Mtume wa Allaah”? Akasema: ((Hicho ni mali bora yetu)). Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.
Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe.
Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:
عن همام (رضي الله عنه) قال: سمعت أبا هريرة (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا أَنْفَقَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ كَسْبِ زَوْجِهَا عَنْ غَيْرِ أَمْرِهِ فَلَهُ نِصْفُ أَجْرِهِ)) - البخاري
Kutoka kwa Hamaam (Radhiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake)) Al-Bukhaariy
4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).
5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Peponi:
عن عبد الرحمن ابن عوف (رضي الله عنه) قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا صَلَّتْ الْمَرْأَةُ خَمْسَهَا، وَصَامَتْ شَهْرَهَا، وَحَفِظَتْ فَرْجَهَا، وَأَطَاعَتْ زَوْجَهَا, قِيلَ لَهَا: ادْخُلِي مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ شِئْتِ)) صحيح الترغيب
Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao)) Swahiyh at-Targhiyb
Hizo ni baadhi ya haki tulizojaaliwa kuzinukuu, tukitaraji kwamba pindi zikitimzwa, basi ndoa itaendelea kudumua katika usalama na amani.
Uoshe(usafishe) moyo wako na utwaharishe.
UOSHE (USAFISHE) MOYO WAKO NA UTWAHARISHE!
قال العلامة ابن عثيمين - رحمه الله تعالى.
Amesema mwanachuoni mkubwa Ibn 'Uthaumin -Allah amrahamu-
فتش قلبك يا أخي،
Uchunguze moyo wako ewe ndugu yangu,
هل فيك رياء؟
Je, kwako kuna (tabia ya) kujionesha?
هل فيك كراهة للحق؟
Je, kwako kuna (tabia ya) kuichukia haki?
هل فيك بغضاء للمؤمنين؟
Je, kwako kuna (tabia ya) kuwabughudhi waumini?
هل فيك حقد على المؤمنين؟
Je, kwako kuna (tabia ya) kuwahusudu waumini?
فإن غسيل القلب كل يوم،
Basi (tambua) kuuosha moyo kila siku,
أهم من غسيل الثياب كل يوم،
Ni muhimu zaidi kuliko kuifua nguo kila siku,
اغسل قلبك وطهره.
Uoshe (usafishe) moyo wako na utwaharishe.
📚 المصدر: اللقاء الشهري (75/2)
[ Chanzo: Alliqaau l-sshahriy (2/75) ]*
Maelezo kutoka kwa mfasiri- Allah amuhifadhi
Usafishe (uoshe) moyo wako na maradhi haya ya moyo ambayo ni maradhi mabaya sana,
maradhi kama hayo aliyoyataja sheikh ambayo mengine ni sababu ya kuvunjika mahusiano na undugu baina ya waislamu,
Huu ni usia mzito mno, kwa sababu tulio wengi sasa hivi tuna maradhi ya nyoyo!! Unaweza ukatuona tumevaa na kupendeza na tunanukia vizuri lakini nyoyo zetu zinanuka na kutoa harufu ya *hasuda, roho mbaya, chuki, mafundo ya moyo, kiburi, kujiona!!*
Kwa ajili hii utaona mizozo haiishi katika safu zetu, na itaendelea kuwepo kama hatutajisafisha nyoyo zetu. ni hatari kubwa muislamu akawa na moyo mchafu!!
( ۚ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ) المائدة: (٤١)
(Hao ndio ambao Allah hakutaka kuzitakasa nyoyo zao (na uchafu wa shirki na kufuru), Watakuwa na udhalili (fedhea) duniani, na akhera watakuwa na adhabu kubwa). [ Al-Maaida (41) ]
*Mfasiri: Abuu Thurayyaa Ismail seiph Mbonde - Allah amuhifadhi*
Dar es salaam, Tanzania 🇹🇿
Mtoto anapopiga chafya.
MTOTO ANAPO PIGA CHAFYA*🎤
قال الشيخ صالح بن فوزان الفوزان حفظه الله :
Amesema Sheikh Swaaleh fauzaan bin Fauzaan- Allah amhifadhi-
"أما الصغير إذا عطس فإنه ﻻ يشمت ولكن يدعو له بالبركة يقال:
Ama mtoto mdogo akipiga chafya hakika haombewi dua (kwa kuambiwa “yarhamuka Allah” lakini ataombewa dua ya Baraka ataambiwa:
بارك الله فيك لأنه عطس طفل عند النبي صلى الله عليه وسلم فقال :
Baaraka Allahu fiika, kwakua alipiga chafya mtoto mbele ya mtume swallah Allahu Alaih wasalam Akasema Mtume:
(بارك الله فيك)
(Baaraka Allahu fiika)
وأمر الطفل إذا عطس أن يحمد الله من باب التعليم."
*Na ama kumuamrisha mtoto anapo piga chafya amhimid Allah (aseme Alhamdulillah) ni katika mlango wa Kumfunza*
📚 المصدر: شرح منظومة الآداب الشرعية (ص٢٨٠)
[ Chanzo: Sharhu Man-ndhuumat Aadaab As-shar'iyyah (ukurasa wa 280) ]
Kwa maana hio watoto wetu khasa wale ambao hawajaanza kusema wakipiga Chafya tunawaambia “Baaraka Allahu fiika”
Ama wale ambao wameanza kuongea tutawaambia waseme “Alhamdulillah” na kisha nasi tutasema Yarhamuka Allah na kisha tutawaeleza waseme “yahdiikumu Allahu wayuslih Baalakum”.
Na Allah ndiye mjuzi zaidi
Hukumu ya kuweka(kupaka) makeup kwa wanawake.
حكم وضع مكياج للنساء!
HUKUMU YA KUWEKA (KUPAKA) MAKEUP💄 KWA WANAWAKE!
سئل ﺍﻟﺸﻴﺦ الإمام الأثري ابن باز - رحمہ الله تعالــﮯ -
Aliulizwa Swali Sheikh imamu mwenye kufuata sunnah Ibn Baaz- Allah aliyetukuka amrahamu-
السؤال:
Suali: 🎤*
ما حكم وضع المكياج على وجه المرأة،
Ni ipi hukumu ya mwanamke kuweka (kupaka) makeup
إذا كانت لا تبدو للأجانب،
Ikiwa hajidhihirishi kwa (wanaume) wa kando,
وإنما تظهر أمام النساء؟
Na hakika si vinginevyo (ikiwa) hudhihiri (huonekana) mbele ya wanawake (wenzake)?
الجواب:
Jawabu: 📚
المكياج إذا كان لا يضر وجهها،
Makeup ikiwa haidhuru uso wake (mwanamke),
لا بأس به،
Basi si vibaya (kuitumia inafaa),
لكن تزيله عند الوضوء،
Lakini aiondoe wakati wa kutawadha,
إذا كان له جسم يمنع الماء،
Ikiwa inaumbile linalozuia maji,
أما إذا كان يضر وجهها،
Ama ikiwa inadhuru uso wake,
يسبب مرضا أو بقعا سوداء،
(Na) inasababisha maradhi au vibaka vyeusi,
أو ما أشبه ذلك،
Au mfano wa hayo,
فإنها تتركه،
*Bila shaka huyo (mwanamke) aiache (asipake),
لأنه حينئذ فيه مضرة،
Kwa sababu (hiyo makeup) muda huo inamadhara ndani yake,
أما إذا كان يجمل وينور،
Ama ikiwa (makeup) ina remba au inang'arisha (uso),
ولكن لا يضر فلا بأس.
Lakini haidhuru, basi hakuna ubaya (kuitumia).
📚 المصدر: فتاوى نور على الدرب (1011)
[ Chimbuko: Fataawa nuur 'aala ddarb (1011) ]
Mfasiri: Abuu Thurayyaa Ismail seiph Mbonde - Allah amuhifadhi
Dar es salaam, Tanzania 🇹🇿
Tuwe waadilifu na twaa: usiongeze wala kupunguza kitu ktk makala hii.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Maulid Bin Swaleh
JINSI ULAJI WA TENDE UNAVYOSAIDIA LEBA YA UZAZI
JINSI ULAJI WA TENDE UNAVYOSAIDIA LEBA YA UZAZI ✍️Abdillah Kitota., MMDSC. وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا...

-
Jaa'far Mponda-Miski ya roho
-
Karibu katika blog hii kwa kupata taarifa mbalimbali juu ya dini ya kiislamu kama vile ,nasheed,qur an,mawaidha na vinginevyo.
-
صيام التاسع مع العاشر أفضل من صيام الحادي عشر مع العاشر. *KUFUNGA (SIKU) YA TISA (9) NA KUMI (10) NI BORA ZAIDI KULIKO KUFUNGA SIKU YA...
-
Imekusanywa na: Ummu Iyyaad Haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: ...